WANANCHI wa
wilayani kilosa mkoani Morogoro wameshauriwa kujiunga na mfuko wa bima ya Afya
CHF ili kupunguza gharama za maisha.
Ameyasema
hayo mkuu wa wilaya ya kiilosa Elias Tarimo June 16 mwaka huu kwenye
maadhimisho ya mtoto wa Afrika ambapo kiwilaya yamefanyika katika kata ya zombo
kijiji cha nyali.
Tarimo
amesema kuwa kwa kutekeleza kauli mbiu hiyo mtoto anatakiwa kukua katika afya
njema na kuwashauri wazazi na walezi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya hiyo
itasaidia kupunguza gharama ya kimaisha kwa kuchangia shilingi elfu tano kwa
kipindi cha mwaka mzima na serikari itachangia mwanachama shilingi elfu
tano na kufikia shilingi elfu kumi.
Aidha
amesema kuwa tatizo la madawa kutopatikana hospitalini ni kutokana na wananchi
wachache kuchangia mfuko huo wa Bima ya Afya CHF na serikali kushidwa kukidhi
hitaji la dawa kwa wananchi,Hivyo amewaomba wananchi kujiunga na mfuko wa Bima
ya Afya ili kuondokana na tatizo hilo la upungufu wa madawa hospitalini.
Naye
meneja wa Mfuko wa Bima ya afya mkoa wa morogoro Bi,Rose Ongara amefafanua kuwa
mwananchi anapaswa kuchangia shiliongi elfu tano kwa kaya yenye watu kumi
na kufafanua kuwa kwa hao watu kumi wote watatibiwa kwa hiyo shilingi elfu tano
kwa kipindi cha mwaka mzima na kueleza kuwa ni sawa na shilingi mia tano kwa
kila mmoja atatibiwa kwa mwaka na kuwataka wananchi kutumia fursa hiyo ili
kujiunga na mfuko huo wa bima ya afya.

No comments:
Post a Comment