![]() |
| Albino aliyenusurika kukatwa viungo mkazi wa Kilombero,Morogoro |
AFISA tarafa ya Manispaa Morogoro Pakalapakala Mlenge,ameahidi
kutokomeza unyanyasaji na unyanyapaa kwa wenye albino katika manispaa ya
Morogoromji licha ya bajeti inayotengwa
dhidi ya mapambano hayo kuwa ndogo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki wakati
akifunga warsha ya wenye ualbino Pakalapakala alisema ili timiza lengo
Halmashauri na serikali zimeamua kufanya tathimini ya utambuzi changamoto
zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi.
Alisema serikali itaendelea kuwajali
watu wenye albino kama walemavu wengine kwa kujitahidi kuzikabili changamoto
zinazo wakabili hususani upatikanaji wa mafuta maalumu,kofia.miwani na mavazi
yanayoendana na halia waliyonayo.
Aidha aliwataka kujishugulisha
kutafuata wafadhili kwa kuandika andiko la mradi kwenye mashirika
mbalimbali wa ndani na nje ili kuziba pengo linalojitokeza pindi serikali
inaposhindwa kutimiza lengo kutokanana uwezo wake kuwa mdogo.
Awali mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino mkoani Morogoro David Mganga alimweleza afisa tarafa huyo kuwa bado halmashauri imeshindwa kutekeleza maazimio waliyokubaliana likiwemo la Afya na elimu kutolewa bure kwao.

No comments:
Post a Comment