![]() |
| Askari wa Kenya wakipakia maiti ndani ya gari |
WATU 20
wameuawa katika shambulizi la pili la usiku katika Pwani ya Kenya huku kundi la
wapiganaji la Alshabaab limekiriki kutekeleza shambulizi hilo la pili katika
vijiji viwili zaidi na kusema kuwa wengi ya waliouwa ni maafisa wa polisi.
Wapiganaji hao walivamia vijiji
viwili karibu na mji wa Mpeketoni ,ambao ni eneo la mashambulizi ya kwanza
ambayo yalisababisha mauaji ya watu 48.
Wakazi wa eneo hilo wamelalamikia
serikali kwa kutowapa ulinzi baada ya shambulizi la kwanza na sasa wanaishi kwa
hofu.
Serikali inasema kuwa wanamgambo wa
Alshabaab walikata mawasiliano ya simu katika eneo hilo kabla ya kutekeleza
shambulizi hilo.
Wanamgambo hao wanaohusishwa na
kundi la Alqaeda wanasema kuwa wataendelea kufanya mashambulizi nchini Kenya
ikiwa serikali haitaondoa wanajeshi wake nchini Somalia.
Shambulizi hilo la vijijini ni
limeonekana kuwa mfumo mpya wa mashambulizi ambayo yamekuwa yakifanya na Al
Shabaab ambalo mara nyingi limekuwa likilenga maeneo ya mijini hasa miji
mikubwa.
Takriban watu 48 waliuawa katika
mashambulizi yaliyofanyika usiku wa kuamkia Jumatatu huku washambuliaji
wakishambulia hoteli na kituo cha polisi pamoja na kuteketeza magari.

No comments:
Post a Comment