![]() |
| Waziri mkuu wa China Li Keqiang (kati) na mkewe Cheng Hong( kulia) akisalimia na waziri mkuu wa Uingereza David Cameroun |
WAZIRI mkuu wa China Li Keqiang amewasili jijini London ,nchini Uingereza ikiwa ni hatua yake ya kwanza kutembelea nchi za Uingereza na Ziara hiyo ya kiongozi huyo wa nchui ya Chini ni ya kwanza toka shike madaraka ikiwa inalenga kugusia masuala ya kiuchumi.
Waziri mkuu huyo atakuwa na mazungumzo na waaziri mkuu wa Uingereza David Cameron na kukutana na malikia wa Uingereza Elizabeth wa pili.\
Aidha waziri mkuu huyi Li anatarajiwa kusaini mikataba yenye thamani zaidi ya dola milioni 30 ukiwa kwenye sekta za miundo mbinu, usafiri wa reli ya mwendo kasi, nishati ya nyuklia na masuala ya fedha.
Li Keqiang ataondoka nchini uingereza siku ya alhamisi akielekea nchini Ugiriki akiwa na ziara ya ya kiofisi ya siku sita ambapo akiwa nchi Ugiriki atatembelea bandari ya Piraeus ambayo imebinafsishwa ambapo kampuni ya bandari toka China inatarajiwa kununua hisa nyingi za bandari hiyo

No comments:
Post a Comment