![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Kilosa Eliasi Tarimo |
MKUU wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo amepiga
marufuku wanafunzi kujishughulisha na biashara yoyote pindi wawapo shuleni na
nyumbani ili kutimiza Sera ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto.
Tarimo
ameyasema hayo Juni 16 mwaka huu katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika
yaliyofanyika Kiwilaya katika Kata ya Zombo
kijiji cha Nyali na kusema kuwa ni marufuku kwa wazazi kuwatuma watoto
kufanya biashara yoyote ile kwani ni kinyume na sheria.
Aidha Tarimo
amesema kuwa wazazi wanawajibu wa kuhakikisha watoto wao wanapata mahitaji yote
muhimu shuleni kama vile madaftari na sare za shule ili kujenga mazingira
rafiki ya kusoma na kujifunza ili kutekeleza mpango wa Serikali wa matokeo
Makubwa Sasa(B.R.N) kwani Elimu ndiyo chachu ya Maendeleo.
Sambamba na hayo amewaasa wazazi kuwapeleka watoto shule kwa kipindi muafaka na kuhakikisha mtoto anakuwa shuleni muda wote wa masomo kwani kila mtoto ana haki ya kupata Elimu bila kujali jinsia wala ulemavu

No comments:
Post a Comment