MKUTANO Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha
Wananchi( CUF) Wilayani Kilosa Mkoani
Morogoro uliokuwa ufanyike juni 15 mwaka huu umehairishwa kutokana na sababu
mbalimbali hadi utakapotajwa tena na Uongozi wa Wilaya.
Hali hiyo
imejidhihirisha katika Ukumbi wa Manyovu uliopo Wilayani Kilosa ambapo ndipo
Uchaguzi ulipangwa kufanyika saa mbili usiku
ili kuweza kuchagua Viongozi mbalimbali wa Wilaya mara baada ya
kushindwa kuhudhuria robo tatu ya wajumbe wa Chama hicho.
Kwa
mujibu wa Mjumbe wa Uchaguzi ngazi ya
Taifa Husein Shaban Mwakikoti amesema kuwa mkutano huo ulikusudiwa kuwa na
wajumbe mia tatu lakini hadi kufikia saa tano usiku wajumbe mia moja na
ishirini tu ndio waliokuwa wamewasili,hali iliyosababisha kuahirishwa kwa
uchaguzi kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho inayosema kuwa
Uchaguzi utafanyika kama kutakuwa na
nusu ya wajumbe wote

No comments:
Post a Comment