![]() |
| Polisi wakikagua ndege ya shirika la ndege la Kenya |
MKUU wa kitengo cha Polisi
katika uwanja wa ndege nchini Kenya , kamanda, Joseph ole Tito, amesema kuwa shughuli
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta zilisitishwa kwa muda
Jumatano asubuhi baada ya maiti ya kijana mdogo kupatikana karibu na eneo la
kurukia ndege.
Maiti
hiyo ilipatikana katika sehemu ya kurukia ndege katika hali ambayo
imewashangaza wengi.
Hata
hivyo alisisitiza kuwa ndege zilizokuwa zinaingia uwanjani humo asubuhi na
mapema hazikuathiriwa na tukio hilo.
Halmashauri
ya huduma za ndege ilisema kuwa uwanja ulifungwa kwa dakika arobaini baada ya
maafisa wa usalama kugundua maiti hiyo.
Kwa
mujibu wa maafisa hao, hatua ya kufunga uwanja huo ilifanywa ili kuondoa mwili
wa kijana huyo.
Ni
ndege ya shirika la ndege la Uturuki tu ndiyo ililazimika kusalia angani kwa
muda huku mwili wa kijana huyo ukiondolewa uwanjani.
Kijana
huyo anaaminika kuwa na umri wa miaka 10 au12 na alikuwa na majeraha upande wa
kushoto wa mwili wake.
''Mwili
wake uliondolewa katika eneo hilo na kwamba uchunguzi unaendelea kufanywa,''
alisema bwana Tito.
Polisi
wamesema watafanya uchunguzi kubaini ikiwa alianguka kutoka kwa gurudumu la
ndege au mtoto huyo alifariki kutokana na sababu nyinginezo.
Pia
miongoni mwa maswali yanayoulizwa ni vipi mwili wake ulipatikana katika uwanja
wa ndege hasa katika njia ya kurukia ndege?
Visa
vya watu kupanda kwenye magurudumu ya ndege kimagendo kwa lengo la kusafiri
kwenda nchi nyingine vimekuwa vikiripotiwa hivi karibuni

No comments:
Post a Comment