![]() |
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo |
HATIMAE usemi wa za mwizi arobaini umemkumba Diwani wa
kata ya Mabwerebwere wilayani Kilosa,akidaiwa kutumia jina na nafasi ya mkuu wa
wilaya hiyo Elias Tarimo kujikusanyia mifugo na fedha kwa wapigakura wake kwa
kisingizio cha kugharimia ugeni na hafla za kitaifa wilayani humo.
Diwani huyo Matei Kayanda(CCM)anadaiwa kunaswa karibuni baada ya
kujitoma kwa mfugaji Teyani Maumbi mkazi wa kijiji cha Kondoa akimtaka ampe
Ng’ombe wawili na shilingi 200,000 zitakazotumika kitoweo kwenye ugeni wa mbio
za Mwenge uliodaiwa kupita wilayani humo Juni 22.
Mkuu wa wilaya hiyo Elias Tarimo amekili kuwepo kwa tukio hilo
alilodai lililenga kumchafua nakuwa tayari mtuhumiwa alitengenezewa mtego
uliomnasa na suala hilo lipo kwenye vyombo vya sheri likiandaliwa utaratibu wa
kupelekewa mahakamani.
Aidha tarimo alisema binafsi amekuwa akikerwa na baadhi ya tabia
ya viongozi kutumia jina na cheo chake kuwadanganya watu kulindwa endapo
watatekeleza kutoa vitu wanavyoombwa na watu wasio na nia njema na yeye nakuwa
anakusudia kuukomesha mtandao huo kwa kuwafikisha kwenye mamlaka za kisheria.
Akisimulia mkasa huo Mfugaji Maumbi alisema siku ya tukio majira
ya asubuhi kuelekea mchana Diwani huyo aliyemgeuza kitegauchumi chake kwa muda
mrefu, alifika nyumbani kwake na kumweleza serikali ya wilaya imekaa na Mkuu wa
wilaya hiyo amemwagiza kufika nyumbani kwa mfugaji kutaka ng’ombe hao na kiasi
hicho cha fedha
Alimtaka haraka afike ofini kwake na alipofika alikuta safu yote
ya utawala akiwemo kamanda wa Takukuru,Usalama wa Taifa, mkuu wapolisi OCD
wilayni humo wakiwa ofisini ambao waliunda mtego uliofanisha kunaswa kwa diwani
huyo.
Juhudi za kumpata diwani huyo Matei Kayanda kutoa ufafanuzi wa
madai hayo zinaendelea licha ya kushindikana baada ya kuizima simu yake ya
kiganjani(0786088870) alipotajiwa anyeeongea nae ni mwandishi wa habari.
Hata hivyo jeshi la polisi kupitia kaimu kamnda wake wa polisi
John Laswai limekanusha kuwepo kwa tukio hilo ingawa aliahidi kuendelea
kufuatilia kwa OCD wilayani Kilosa.
No comments:
Post a Comment