![]() |
Wajumbe wa bunge la katiba |
UMOJAwa Vijana
wilayani Kilosa mkoani Morogoro unaandaa kongamano huru ili kuweza kuhamasisha
kupata katiba bora itakayokuwa na tija kwa Taifa kwa ujumla.
Hayo
yameelezwa juni 27 mwaka huu na Rais wa Umoja huo Denis Nyiraha katika
mbiu ya maendeleo ambapo amesema wameamua kuanzisha umoja huo ili kuweza
kufikisha kwa watu wote kuwa na uelewa juu ya suala zima la katiba.
Nyiraha
amesema kuwa kongamano hilo linatarajia kufanyika hivi karibuni ili kuweza
kutoa fulsa kwa wananchi kutoa maoni yao lakini pia kuweza kurudisha Uzalendo
wa Taifa la Tanzania kwa ujumla.
Aidha
Nyiraha ametoa wito kwa jamii kuweza kushiriki katika mchakato huo ili kusaidia
kurejesha jitihada za uzalendo wa Mtanzania lakini pia kufanikisha kupata
katiba bora ambayo itakuwa ni ya miaka hamsini ijayo.
Naye
aliyejitambulisha kwa jina la Charles Golaga ameupongeza mfumo huo na kusema
kuwa ni mzuri kwani una manufaa katika jamii ya lakini ameweza kuwashauri
wanachama hao kuweza kuepuka siasa na badala yake uwajibikaji uwepo.
No comments:
Post a Comment