![]() |
Rais Hassan Rouhan wa Iran akiongea na vyombo vya habari |
RAIS Hassan
Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amewatumia salamu za pongezi viongozi wa
nchi zote za Kiislamu duniani kwa munasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani ambapo amewataka wautangaze mwezi wa Ramadhani mwaka huu kuwa ni
'Ramadhani ya Amani na Rahma'.
Aidha amewataka viongozi wa nchi za Kiislamu
kujitahidi kuleta umoja na udugu miongoni mwa Waislamu kote duniani.
Katika
ujumbe wake huo, Rais Rouhani amesema Ramadhani ni mwezi wa saumu, kiyamu na
rehma na ibada na hivyo viongozi wa Kiislamu wanapaswa kuchukua hatua za
kuimarisha umoja wa Kiislamu.
Katika sehemu ya ujumbe wake, Dkt. Rouhani
ameseama: 'Mwaka huu, Waislamu wanaukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku
machafuko na misimamo mikali ikiusukuma ulimwengu wa Kiislamu katika hofu,
ujahili, na ghadhabu mambo ambayo yanawaandalia maadui njia ya kutekeleza njama
zao za jadi za kuwafarakanisha Waislamu sambamba na kuibua vita vya kimadhehebu
na kikaumu."
No comments:
Post a Comment