WAZEE katika baadhi ya nchi huheshimika na kuwa
akiba ya busara kwa kizazi cha vijana na zaidi ya yote huangaliwa na kusaidiwa
kimaisha.
Huko
nchini Korea Kusini maisha kwa wazee ambao walichangia katika uchumi wa Taifa
hilo na ustawi wa taifa hivi sasa wanaishi katika mazingira magumu hali ambayo
kwa wanawake wazee inawalazimu kubuni mbinu mpya za maisha kwa kujitumbukiza
katika biashara haramu ya ngono kwa kuuza miili yao ili waweze kujipatia fedha
za kuendesha maisha yao ya kila siku.
Taarifa
hizo zinajuza kuwa, katika nchi zilizo nyingi na hata Afrika mashariki biashara
ya ngono hufanywa na wasichana wadogo na hata wa umri wa kati kwa lengo la
kujipatia kipato .
Akiwa
amevalia koti lake jekundu,na kupaka rangi ya mdomo kwa ustadi Bi. Kim Uen Ja
mwenye umri wa miaka 71 mavazi yake yanabainisha wazi kwamba angependa kuwa na
muonekano wa msichana mdogo na mrembo, yupo katika eneo la kupumnzika la
Jongno-3 subway station huku pembeni mwake akiwa na begi kubwa lililosheheni
chupa ndani yake.
Bi.
Kim ni mmoja kati ya wanawake wazee wa Korea ya kusini ambao hupendelewa kuuza
kinywaji ambacho wanaume wanasema kinawaongezea nguvu kijulikanacho kwa jina la
Bacchus, lakini wanawake hawa wanaouza vinywaji hivi baadhi yao ni wale wenye
malengo ya kujiuza ili wapate fedha za kuendeshea maisha yao.
No comments:
Post a Comment