![]() |
Wakinamama wakinyonyesha |
HIVI KARIBUNI, ilikosolewa kwa kuondoa picha ya wapenzi wawili wa jinsia
moja wakibusiana , baada ya mtu kusema kuwa picha hizo ni za kukera.
Lakini
swala la hivi karibuni ambalo limejadiliwa sana kuhusiana na picha kwenye
mtandao huo wa kijamii, ni kuhusu mama mmoja aliyekuwa akimnyonyesha mwanawe
hadharani na kuweka picha hiyo kwenye akaunti yake.
Baadhi
walisema picha hiyo ilikuwa ya uchi mno na kwamba iliwakera watu wengi sana.
Sasa
hivi Facebook imebadilisha sheria zake kuhusu picha za wanawake wakiwanyonyesha
watoto wao.
Katika
sehemu ya mtandao huo , maagizo sasa yanasema kuwa ''Ndio tunaruhusu picha za
wanawake wakiwanyonyesha watoto wao ni jambo zuri na ambalo hatuwezi kulikosoa.
Ni vyema kujua kuwa ni muhimu kwa akina mama kuonyesha watu picha hizo kwenye
Facebook. Picha hizi sasa zinaruhusiwa.''
Facebook
inasisitiza kuwa mabadiliko yoyote wanayofanyia sera zake kuhusu picha,
hutokana na malalamiko ya watumiaji wa mtandao huo.
Katika
nchi nyingi za Ulaya, wanawake wengi huogopa kunyonyesha hadharani kutokana na
unyanyapaa. Wanawake nchini Uingereza waliwahi kuandamana wakipinga unyanyapaa
unaojitokeza kwa wanawake ambao hunyonyesha watoto wao hadharani.
Swala
la kuwanyonyesha watoto hadharani sio hoja kwa wanawake wengi barani Afrika
kwani kwao pale ambapo mtoto analilia Titi mama hutafuta mahala safi na
kumnyonyeshea mtoto wake.
No comments:
Post a Comment