![]() |
Wanajeshi wa Uingereza |
UINGEREZA imesema
kuwa inafanya mazungumzo na kenya ili kutatua mzozo kuhusu mafunzo ya wanajeshi
wa Uingereza nchini humo.
Serikali
ya Kenya inaaminika kuchelewa kuwaruhusu wanajeshi zaidi wa Uingereza kuingia
nchini humo ili kufanya mazoezi.
Maelfu
ya wanajeshi wa Uingereza huzuru nchini kenya kila mwaka kwa mafunzo ya wiki
sita lakini hilo limesitishwa kwa mda baada ya kenya kuchelewa kutoa ruhusa ya
kidiplomasia kwa ndege inayowabeba wanajeshi wanaotarajiwa kufanya mafunzo
hayo.
Hatua
hiyo inaonekana kama kulipiza kisasi kwa tahadhari ya kusafiri humu nchini iliotolewa
na serikali ya Uingereza kwa raia wake ambayo imeathiri pakubwa sekta ya utalii
nchini.
Wanajeshi
wa Uingereza wamekuwa wakifanya mafunzo nchini kwa zaidi ya miongo minne lakini
makubaliano kati ya mataifa hayo mawili kuhusu mafunzi hayo yanakamilika mwezi
Aprili.
Maseneta
kutoka upande wa chama tawala nchini kenya wamemtaka rais Uhuru kenyatta
kutotia sahihi mkataba mpya.
No comments:
Post a Comment