![]() |
Mkuu wa wilaya ya Kilosa Elias Tarimo |
ZAIDI ya wakazi mia mbili waliokesha kwenye mkesha
wa Mwenge wa Uhuru juni 23 mwaka huu katika Kata ya Kisanga Wilayani Kilosa
Mkoani Morogoro ni asilimia 3.5 ndiyo waliokutwa na maambukizi ya virusi vya
UKIMWI na vimelea vya ugonjwa wa malaria
Hayo
yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Elias Tarimo kabla ya kukabidhi
Mwenge wa Uhuru ngazi ya Mkoa mara baada ya kumaliza mkesha Kata ya Kisanga
juni 24 mwaka huu, pia amesema katika tathimini hiyo iliyotolewa ni kwa sababu
ya mwitikio chanya kwa wananchi kujitokeza kupima kwa hiari .
Aidha
Tarimo amesema kuwa jumla ya waliojitokeza kupima virusi vya UKIMWI ni 325 tu
ambapo wanaume 182 na wanawake 143, huku wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI
ni 8 wanaume 3 na wanawake 5 ambayo ni sawa na asilimia 2.5, pia waliopima
malaria 287 wanawake 138 wanaume 149 waliokutwa na vimelea vya malaria ni 30
sawa na asilimia 1.1 na wamepatiwa maelekezo sahihi ya kutumia dawa za malaria
na kisha kukabidhi Mwenge kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Hata
hivyo Mkuu wa MKoa wa Morogoro Joel Bendera amesema kuwa ameupokea Mwenge ukiwa
salama na ameukabidhi mkoa wa
Iringa kwa Mkuu wa Mkoa Christine Ishengoma na amewasisitiza wananchi
kuzingatia ujumbe wa Mwenge usemao Katiba ni sheria kuu ya nchi chini ya kauli
mbiu isemayo Jitokeze kupiga kura ya maoni tupate katiba mpya.
Ameongeza
kwa kusema kuwa wananchi wanapaswa kuacha kufanya marumbano yasiyo na msingi hali
ambayo itazorotesha maendeleo ya jamii pia kutumia vyandarua vyenye dawa ili
kufikia lengo la Tanzania bila malaria inawezekana na mara ujihisipo na dalili
za malaria wahi kituo cha Afya ukapate huduma na Tanzania bila UKIMWI
inawezekana jitokeze kupima kwa hiari ili kutokomeza maabukizi mapya ya virusi
vya UKIMWI.
No comments:
Post a Comment