![]() |
Mwenyekiti wa bunge la katiba Samuel Sitta |
WITO umetolewa
kwa wote wanaohusika katika mchakato wa kupata katiba mpya kungalia maslahi ya
Taifa kwanza badala ya kuangalia maslahi binafsi au ya vyama vyao.
Hayo
yamesemwa na Afisa wa shirika la Oxfam nafasi za wanawake katika kupata Katiba Mpya
Heri Ayubu wakati wa mdahalo wa mchakato wa katiba na jinsia uliofanyika Juni
26 na kuwahusisha Wanawake mbalimbali kutoka tarafa ya Kilosa.
Ayubu
amesema tangu kuanza kwa mchakato wa kupata katiba Mpya kumekuwepo na
changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya makundi kuvutia kwake hususani watu wa
vyama vya siasa hali inayotoa mashaka ya kupatikana kwa katiba nzuri
iliyopendekezwa na wananchi.
Aidha
ayubu ameongeza kusema kuwa wanaendelea kutoa elimu mbalimbali kwa wadau
hususani wanawake ili muda utakapofika wakati wa kupiga kura ya katiba
wawe na ufahamu mkubwa ju ya katiba hiyo maamuzi watakayotoa yawe sahihi.
Kwa
upande wa wajumbe waliohudhulia mdahalo huo mwalimu Sikudhani Mfinanga na
Rehema Mhini kwa niaba ya wanawake wenzao wamesema kuwa wanashukuru kwa
kufanyika kwa mdahalo kwani umeweza kuwapanua kifikra na wamewaomba wajumbe wa
bunge maalumu la katiba kuheshimu mawazo yao na kutoa wito kwa wanawake nchi
kuisoma kwa makini katiba mpya itakapotoka na kujitokeza katika kuipigia kura.
Mdahalo
huo umeandaliwa na shirika la msaada wa kisheria Morogoro Palaregal kwa
kushirikiana na mashirika ya Restress Development.
No comments:
Post a Comment