![]() |
Mzee akisaidiwa kupiga kura nchini Libya |
WAKILI mashuhuri ambaye pia ni mkereketwa wa haki za kibinadamu
nchini Libya ameuliwa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika mji wa
Benghazi nchini Libya jana, Jumatano.
Mauaji hayo yametokea baada ya
uchaguzi wa Wabunge - ambao wengi walidhani utapunguza visa vya utovu wa
usalama.
Wakili huyo mwanamke, anayejulikana
sana kwa kupigania haki za wanawake na uhuru wa kisiasa alionekana mara ya
mwisho akipiga kura jana.
Salwa Bughaighis alishambulia
nyumbani kwake jana jioni.
Ripoti kutoka Benghazi zinasema
alishambuliwa na watu waliokuwa na bunduki waliokuwa wamefunika nyuso zao.
Matabibu kutoka hospitali ya
Benghazi alikokufia walithibitisha kuwa alikufa kutokana na majeraha ya risasi
aliyokuwa nayo kichwani.
Jamii zake wanaamini ametekwa nyara
ingawa haijulikani kwa hakika alivyotoweka.
Watu wengi waliosikia habari za kufa
wakili huyo wameeleza masikitiko na hasira zao kupitia vyombo vya habari na
mitandao ya kijamii.
Alikuwa miongoni mwa mawakili wa
kwanza na mkereketwa aliyepinga kutiwa mbaroni mara kwa mara kwa waandamanaji
waliokuwa wakimpinga aliyekuwa mtawala wa Libya, Muamar Gadhafi.
No comments:
Post a Comment