Tuesday, June 10, 2014

HALMASHAURI za miji, manispaa na majiji nchini zatakiwa kutenga bajeti kwaajili ya walemavu




CHAMA cha watu wenye ulemavu nchini TAS kimezitaka halmashauri za miji,manispaa na majiji nchini kutenga bajeti za kutosha kukabiliana na changamoto zinazowakabili wenye ulemavu wa ngozi.


Akizungumza kwenye tathmini ya ushawishi na utetezi  mjini iliyofanyika mjini Morogoro, Katibu mkuu wa chama cha watu wenye ualbinoTanzaia (TAS) Ziada Ally alisema watu wengi wenye tatizo hilo wanaathirika kwa kutokuwa na uwezo.

Akitaja baadhi ya chamngamoto zinazo wakabili na mahitaji yao zaida kuwa ni pamoja na vilinda miili yao kama vile mafuta kofia bila kusahau huduma za matibabu kutokana wengi wao kutokuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo .

Katika mahitaji hayo alisema kila wilaya kuweka mikakati ya kutenga bajeti ya jamii hiyo na kukumbushana  kila wanapokaa vikao wajaribu kuweka msisitizo juu ya walemavu  hao.

No comments:

Post a Comment