Tuesday, June 10, 2014

INUKA yawashajiisha wadau mbalimbali wa maendeleo kujitokeza kugharimia saratani ya shingo






MKURUGENZI  wa Taasisi ya maendeleo ya wanawake (INUKA)David Msuya amewataka wadau mbalimbali  wa maendeleo ya wanawake kujitokeza kugharimia elimu ya saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake.


Akizungumza kwenye semina ya walimu iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kata  ya Dakawa wilayani Mvomero, mkoani Morogoro  Msuya alisema tatizo la saratani ya kizazi limekuwa kubwa hasa kwa watu walioko vijijini kutokana na kukosa huduma ya afya inavyotakiwa.

Alisema ikiwa wadau mbalimbali watashiriki kutoa elimu ya salatani ya kizazi ugonjwa huo unaweza kutokomezwa.

 Kwa mujibu wa Msuya INUKA imejipanga kutoa  elimu ya salatani ya shingo ya kizazi  kwa walimu wa shule za msingi waliopo mikoa ya Morogoro na Iringa.


No comments:

Post a Comment