IMEELEZWA kuwa zaidi ya shilingi milioni kumi na sita zimekusanywa
katika maandalizi ya kuupokea mwenge wa uhuru wilayani kilosa mkoa wa Morogoro
kutoka sehemu mbalimbali wilayani humo.
Hayo
ameelezwa na mwenyekiti wa kikao hicho cha kamati ya sherehe za mwenge Elias
Tarimo ambaye ni mkuu wa wilaya ya kilosa kilichofanyika wilayani kilosa kwenye
ukumbi wa mikutano wa Halmashuri mwishoni mwa wiki iliyopita.
Aidha
Tarimo amewataka wakuu wa idara na watendaji wa kata kuwahimiza waliochini yao
kuchanga michango hiyo ili kufanikisha sherehe hizo za mbio za mwenge.
Amesema
mwenge wa uhuru unatarajiwa kupokelewa june 23 mwaka huu ukitokea kilombero ukiwa
umebeba ujumbe usemao” Katiba ni sheria kuu ya nchi “wenye kauli mbiu isemayo JITOKEZE
KUPIGA KURA YA MAONI ILI TUPATE KATIBA MPYA ambapo utazindua miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Mkuu
wa wilaya ameongeza kusema kuwa miradi itayofunguliwa na mwenge ni pamoja na
Hostel ya sekondari ya Kisanga kituo cha uhamasishaji wa kupima ukimwi ulaya na
kuweka jiwe la msingi kwa kituo cha wakulima Isanga
.
No comments:
Post a Comment