WATOTO mapacha wenye
umri wa miaka sita wamekufa baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji wakati
wakicheza katika kijiji cha Pipani, tarafa ya Kiwangwa , wilaya ya Bagamoyo
mkoani Pwani.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Pwani Ulrchi Matei amesema watoto hao wametumbukia kwenye
kisima kilichojirani na nyumbani kwao ambapo baada ya pacha wa kwanza kuona
mwenzake anazama alikwenda na kutaka kumuokoa ndipo naye alipozama.
Kwa
mujibu wa kamanda huyo tukio hilo la june 8 mwaka huu majira ya saa kumi jioni
katika kijiji cha pipani kiwangwa kata ya kiwangwa tarafa ya msata wilaya ya
bagamoyo.
Ameeleza
kuwa miili ya watoto hao mapacha baada ya kuopolewa ilikabidhiwa kwa ndugu kwa
ajili ya maziko .
No comments:
Post a Comment