ITALIA yakiuka sheria za kimataifa za watoto
NCHI ya Itali imeelezwa kukiuka haki za watoto kwa kuwafanyisha
kazi kwa nguvu makumi ya maelfu ya watoto nchini humo,jambo linalokiuka sheria za
kimataifa za haki ya mtoto.
Ripoti iliyotolewa na shirika la
umoja wa mataifa linaloshughulikia watoto UNICEF limeeleza kuwa takribani
watoto 260,000 wanalazimishwa kufanya kazi zinazohatarisha afya na saikolojia zao
huku wakilazimishwa kufanya kazi ngumu wale wenye umri chini ya miaka 14
.Kwa mujibu wa ripoti hiyo
watoto hufanya kazi mwenye baa,hoteli,kwenye mashamba na wengine kufanya kazi
ya kusambaza makaratasi ya matangazo ya biashara.
Ukikukwaji huo unafnyika zaidi
kusini mwa nchi ya Italia.
No comments:
Post a Comment