MAADHIMISHO
ya siku ya mazingira Wilayani Kilosa yamefanyika hapoa jana katika tarafa ya Magole
kijiji cha Mbigiri Wilayani Kilosa, mkoani Morogoro.
Hayo
yameelezwa na kaimu afisa na mazingira Brayson Shoo ofisini kwake alipokuwa
akiongea na mbiu ya maendeleo ambapo amesema kuwa sababu hasa ya kufanyia
maadhimisho hayo tarafa hiyo ni kutokana na janga la mafuriko lililotokea hivi
karibuni tarafani humo ili wananchi waweze kujifunza jinsi ya kutunza
mazingira.
Pia
amesema kazi za usafi wa mazingira zimeanza huko Magole ikiwa ni pamoja na
kupulizia dawa ya kuua wadudu kama mbu na wengineo kwenye kambi za wahanga na
zinafanyika .
Aidha
Shoo amesema kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkurugenzi wa halmashauri ya
wilaya ya Kilosa na kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ni “TUNZA MAZINGIRA ILI
KUKABILIANA NA MABADILIKOYA TABIA YA NCHI”.
No comments:
Post a Comment