WANAWAKE Mkoani Morogoro wametakiwa kutokata tamaa katika shughuli
za kiuchumi ili kuondokana na utegemezi pia ombaomba kwa wanaume zao na jamii.
Ushauri huo umetolewa na
mwenyekiti wa umoja wa wanawake mkoa wa Morogoro Mariam Kyamani kwenye sherehe
ya miaka 10 ya kikundi cha kijamii cha Upendo Women Group kilichopo kata
na mtaa wa Tubuyu manispa ya Morogoro.
Kyamani ambaye pia ni diwani wa kata
ya Kingolwila alisema dhana ya mwanamke kuendelea kuwa tegemezi imepitwa na
wakati badala yake wanatakiwa kujishugulisha kulimngana na flsa walizonazo.
Katika risala ya kikundi hicho
pamoja na mambo mengine iliomba mashirika na taasisi mbalimbali kuendelea
kusaidia vikudi vya kijamii kwa ajili ya kuleta mabadiliko ya kinamama ya
kiuchumi.
No comments:
Post a Comment