MAMLAKA ya chakula na Dawa (TFDA) imesema kati ya
machinjio zaidi ya 900 yaliyopo nchini ni 20 pekee yamesajiliwa jambo ambalo
linalochangia uwepo wa huduma mbovu zisizozingatia viwango vinavyotakiwa.
Hayo
yamesemwa ivi karibuni jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa TFDA Raymond
Wigenge wakati akizungumza na mbiu ya maendeleo mara baada ya kufungua semina
ya siku mbili kwa wajasiriamali wadogo wa vyakula kutoka mikoa mbalimbali
nchini.
Wigenge
aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu katika ufunguzi wa semina hiyo amesema TFDA
inatambua changamoto zinazoikabili sekta ya nyama , ikiwemo uchafu na
miundimbinu katika machinjio na imejiandaa kuweka mikakati mipya kupambana na
hali hiyo.
Amesema
TFDA imetoa agizo la maboresho zaidi ya miaka mitatu iliyopita na sasa inaandaa
mikakati kuleta mapinduzi katika sekta ya nyama hasa machinjio ili kuboresha
huduma , afya ya jamii na kuhakikisha sheria na miongozoinazingatiwa.
No comments:
Post a Comment