WANANCHI Wilaya
ya Kilosa Mkoani Morogoro , wametakiwa kuacha kutupa taka nje ya Dampo
zilizojengwa kwa ajili ya kutupa taka hizo kwani ni hatari na inweza
kuleta milipuko ya magonjwa.
Hayo
yameelezwa na kaimu Afisa Usafi Wilaya ya KIlosa MUHAMMADI MUHOMBORAGE hivi
karibuni ofisi kwake wakati akiongea na Mbiu ya Maendeleo ambapo amesema
kuwa kuna Baadhi ya wafanya Biashara hutupa uchafu nje ya dampo maarufu
kwa jina Vizimba wakati wa usiku na kusababisha taka hizo kuzagaa hovyo.
Aidha
Muhomedi Muhomborage akiongea suala la wanaotupa taka nje ya vizimba nyakati za
usiku amesema umewekwa mkakati kuweza kuwabaini na kuwakamata watu hao na
ambapo hatua kali zita chukuliwa dhidi yao.
Ameongeza
kusema kuwa mtu yoyote atakaekamatwa akitupa ovyo taka nje ya kizimba hatozwa
faini papohapo na kufikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment