Saturday, June 7, 2014

WAFANYABIASHARA waaswa kufunga maduka mapema ili kuepusha kuvamiwa na majambazi



JESHI la polisi Wilaya Kilosa Mkoani Morogoro limetoa wito kwa wafanyabiashara wenye MADUKA MAKUBWA kufunga mapema maduka yao ili kuepusha kuvamiwa na majambazi .
Wito huo umetolewa mapema jana na Mkuu wa Polisi (OCD) Wilaya ya kilosa  BREKI MAGESA wakati akizungumza na Mbiu ya Maendeleo ofisini  kwake.


OCD MAGESA amesema kuwa kwa hali ya sasa hali si shwari kwenye jamii ambayo imechanganyika na watu wabaya ambao wamekuwa wanafanya uhalifu usiku kwa kuvamia kwenye maduka na kupora fedha na vitu mbalimbali .

Amesema kuwa wanapaswa  wafunge maduka yao angalau ifikapo saa moja jioni kukiwa kweupe  bado na mwanga ili kuepusha vivutio vya waarifu  kwani kufunga maduka yao usiku giza limeingia husababisha kumpa mwanya muharifu kuvamia na hata kumtambua muharifu huyo inakua ngumu kutokana na giza.
Mapema hivi karibuni majambazi yakiwa na siraha yalivamia maduka usiku wa saa tatu maeneo ya Kimamba na kupora fedha na simu kwa wafanya biashara wenye maduka.

No comments:

Post a Comment