Saturday, June 7, 2014

SERIKALI yaombwa kupeleleka wataalamu wa mazingira katika machimbo ya dhahabu wilayani Ngorogoro



WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha, wameikumbusha serikali kuwapeleka wataaalamu wa mazinigra wa kutosha katika machimbo hayo ili kuunusuru eneo la machimbo kutokana na uharibu wa mazingira.

Wakiongea na waandishi wa habari mjini Ngorongoro mapema jana, wachambaji haowameeeleza kuwa,wachimbaji wengi wanachojali ni kupata dhahabu bila ya kuangalia athari zinazopatikana baada ya kumalizika kwa shughuli za uchimbaji.

Wamesema , ni muhimu kwa wizara yavnishati namadini kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya kuleta wataalamu wa kutosha wa mazingira kutoa elimuna uraghibishi unaowezeshwa wachimbaji kutekeleza mikakati ya kupambana na uharibifu wa mazingira.

Kwa mujibu wa taarifu za hivi karibuni toka vyanzo mbalimbali vya habari ni kuwa zaidi ya wachimbaji wadogo 7000 wamevamia kijiji cha Samunge ,wilaya Ngorongoro, kwaajili ya uchimbaji wa madini ya dhahabu.


No comments:

Post a Comment