SERIKALI imeombwa
kujenga uzio wa tofari katika hospitali ya wilaya yaKilosa, mkoani Morogoro,ili
kuepusha uchafuzi wa mazingira kutokana na tabia ya baadhi ya wananchi
wanaotupa taka kando kando ya hospitali hiyo.
Ombi
hilo limetolewa hivi karibuni na Afisa
Afya wa wilaya ya Kilosa Bi Rose Nguruwe
wakati wa wiki ya kuadhimisho siku ya mazingira
duniani.
Amesema
hospitali ya wilaya inakabiliwa na changamoto
ya wananchi kutupataka ovyo katika eneo
la jirani na hospittali hali inayohatarisha afya ya wananchi nawagonjwa waliopo
katika eneo hilo.
Hata
hivyo Bi Rose amelipongeza jeshi la magereza wilayani humo kwa kushiriki
kikamilifu katika maadhimisho ya wiki mazingira kwa kufanya usafi katika maeneo
mbalimbali ya hospitali ya wilaya.
No comments:
Post a Comment