WAKULIMA wa zao la muhogo mkoani Mtwara, wameipongeza
Taasisi ya kimataifa ya utafiti na uendelezaji wa zao la muhogo (IITA)kwa
jitihada zake za kuwasaidia wakulima wa zao hilo mkoani humo.
Wakiongea
na mbiu ya maendeleo mapema leo , wakulima hao wameeleza kuwa Taasisi hiyo
ifanya kazi kubwa ya kuchangia maendeleo ya wakulima wa muhogo ikiwa nipamoja
nakutoa elimu ya namana ya kupambana na magonjwa na wadudu waharibifu wa zao
hilo, utengenezaji wa bidhaa zitokanazo na muhogo na elimu ya namna ya kutatauta
masoko ya bidhaa hizo.
Taasisi
ya International Institute of Tropical Agriculture(IITA) iliyopo Mikocheni
jijini Dar es salaam inatoa mchango mkubwa wa kukuza zao la muhog kwa kufanya
tafiti na kuiwaezesha wakulima wa zao hilo katika mikoa mbalimbali hapa nchini
ukiwemo mkoa wa Mtwara.
Mkoa
wa Mtwara ni miongoni mwa mikoa iliyopo katika mpango maalum wa Taasisi hiyo wa kuwaezesha wakulima wa zao
la muhogo kupambana na umaskini wa
kipato.
No comments:
Post a Comment