POLISI jamii
wametakiwa kuwa waadilifu na uwaminifu katika utendaji wao wa kaziza kila siku .
Ushauri huo umetolewa mapema jana na
mpelelezi mkuu wa makosa ya jinai Wilayani Kilosa,mkoani Morogoro Peter Nsanto wakati akiwakabidhi vitambulisho
polisi jamii 26 wa kikundi cha mapambano group katika kijiji cha Ulaya mbuyuni
kata ya ulaya wilayani kilosa.
Ameongeza kuwa amefarijika sana
baada ya kuwaona polisi jamii hao wakiwa na nia ya kufanya kazi kwa kujitoa kwa
nguvu zote na kusema kuwa vitambulisho walivyopata vitawasaidia katika
utendaji wao wa kazi pia amewaasa polisi jamii hao kuwa kioo kizuri katika
jamii kwa kujiepusha na vitendo viovu na badala yake wawe mfano mzuri katika
jamii .
Kwa upande wake kamanda msimamizi
tarafa ya Ulaya Sir. Agent Mohamed wa kata ya Ulaya amesema kuwa kampeni hii ya
polisi jamii imesaidia sana kupunguza mlundikano mkubwa wa kesi
mahakamani kwani kesi nyingi zitatatuliwa ngazi ya vijiji tofauti na
ilivyokuwa mwanzo kwa kila kesi kupelekwa polisi.
Aidha mtendaji kata , kata ya Ulaya Hassani
Kutundumu amefarijika sana kwa vijana hao wa polisi jamii kwa kupatiwa
vitambulisho hivyo na amewataka polisi jamii hao kufuata maadili na utaratibu
walizofundishwa jinsi ya ukamataji sala
No comments:
Post a Comment