Sunday, June 8, 2014

WATENDAJI wa ngazi za juu serikalini ndio chanzo cha migogoro ya ardhi vijijini, Imebainika



CHANZO cha migogoro ya ardhi isiyoisha katika vijiji mkoani Morogoro kimebainika kuchochewa na vijikaratasi na vibali vyenye maagizo kutoka kwa vigogo wenye mamlaka serikalini vikitaka wananchi na viongozi wa vijiji kutopuuza badala yake watekeleze yaliyo kwenye vikaratasi hivyo.
 Hayo yaliibuliwa mwishoni mwa wiki kwenye mafunzo ya siku tatu kuhusu sera na sheria za ardhi kwa wenyeviti,watendaji,makundi maalumu wakiwemo wakulima na wafugaji wa vijiji vya kata ya Maguha na Magubike wilayani Gairo,mkoani MorogoroKilosa yaliyoandali na asasi ya Dira Theatre Group na Foundation for civil society .


Walisema migogoro katika vijiji mkoani Morogoro inatokana na wananchi kutoshirikishwa katika utwaaji maeneo, uwekezaji usio na tija,vijikaratasi vitokanavyo na ubabe na nafasi walizonazo vigogo maofisini na uelewa mdogo walionao viongozi wa vijiji na wanachi juu ya masuala ya ardhi.

Aidha waliongeza kuwa changamoto nyingine inayochangia migogoro ni umasikini walionao wanachi ambao umekuwa kichocheo kikubwa cha uuzwaji ardhi bila hata kufuta misingi na taratibu yenye tija kwao na jamii zinazowazunguka.




No comments:

Post a Comment