Wednesday, June 25, 2014

SERIKALI yatakiwa kupanga bei ya mazao ya wakulima ili kuleta tija


Wakulima wakiuza mazao sokoni

WITO umetolewa kwa Serikali kupanga bei maalumu kwa wakulima itakayo weza kuleta tija pindi watakapo vuna mazao yao hali itakayo pelekea kuepukana na bei za wafanya biashara ili waweze kujikwamua kiuchumi.


Wito huo umetolewamapema  jana na wananchi wa wilayani kilosa,mkoani Morogoro wakati wakiongea katika kikao walichokaa na waandishi wa habari kujadili mada iliyokuwa ikisema ni kipaumbele gani kimetolewa kwa wakulima juu ya mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN).

Mmoja wa wananchi hao kutoka Mgeta,iwlayani Mvomero  ambaye hatukuweza kupata jina lake amesema  kuwa bei wanayouzia mazao yao inapangwa na wafanya biashara   kwani bei zao haziendani  na gharama za uzalishaji hivyo kushindwa kuendesha maisha yao na kubaki kuwa watu wa maisha duni.

Mwananchi huyo amefafa kuwa Serikali inatakiwa kuweka mikakati ya bei ya mazao  ya wakulima kama ilivyo kwa wafanya biashara  ili waweze kuepukana na umasikini kupitia kilimo.

No comments:

Post a Comment