![]() |
Madaktari nchini Siera leone wakipulizia dawa |
SIERA LEONE imeonya kuwa ni
uhalifu mkubwa kwa mtu yeyote kuwapatia maficho watu wanaougua ugonjwa wa
ebola.
Wizara ya afya
imesema kuwa wagonjwa kadhaa wametoroka katika hospitali katika wilaya ya
Kenema,ambayo ndio eneo la kwanza la kuzuka ugonjwa huo.
Shirika la afya
Duniani WHO limetaka hatua za haraka kuchukuliwa ili kudhibiti maambukizi ya
ugonjwa wa ebola katika mataifa ya Magharibi ambao umewaua takriban watu 400.Ni
ugonjwa wenye idadi kuu ya visa,vifo na ueneaji.
kumekuwa na visa
600 vya ugonjwa huo nchini Guinea ambapo mkurupuko huo ulianza miezi minne
iliopita pamoja na mataifa jirani ya Sierra Leone na Liberia.
Asilimia 60 ya
raia walioambukizwa na virusi vya ugonjwa huo wamepoteza maisha yao.
Harakati
za kuthibiti usambaaji wa ugonjwa wa ebola zaendelea
Shirika la afya
duniani linasema kuwa nchini Sierra Leone pekee kumekuwa na vifo 46 kati ya
watu 176 walioambukizwa ugonjwa huo.WHO tayari imewatuma wataalam 150 katika
eneo hilo ili kusaidia kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo.
Daktari Shek Moar
Khan ambaye anawahudumia wagonjwa wa ebola katika hospitali kuu ya kanema
amesema kuwa maafisa wake walikabiliwa na pingamizi wakati walipojaribu
kuwaelezea wakaazi kuhusu ugonjwa huo.
Wafanyikazi wa
idara ya afya nchini humo wamekuwa wakijaribu kuwaelezea raia katika maeneo
ambayo yameathirika kwamba ''ugonjwa huo si wa siri na kwamba ni ugonjwa ambao
unaweza kuambukizwa, na iwapo wangeweza kusikiza ushauri wetu basi tungepunguza
usambazaji wa ugonjwa huo'',alisema.
Siku ya ijumaa
shirika hilo la afya liliyaambia mataifa ya afrika magharibi kama vile Ivory
Coast,Mali,Senegal na Guinea Bissau kujiandaa kwa wageni walio na maambukizi ya
ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment