![]() |
Bacary Sagna |
WAKATI wafuasi
wa dini tukufu ya Kiislamu duniani kote wameshaanza kuufunga mwezi mtukufu wa
Ramadhani.
Bacary Sagna beki wa timu ya taifa ya Ufaransa ameeleza
kinagaubaga kwamba, ataendelea kufunga saumu ya mwezi huo, licha ya kukabiliwa
na kibarua kigumu cha mashindano ya kombe la dunia ambayo yameingia hatua ya
pili ya mtoano.
Sagna amesisistiza kwamba, ataendelea kufunga
saumu ya mwezi mtukufu, licha ya kukabiliwa na mechi ngumu kwenye michuano hiyo.
Ameviambia vyombo vya habari vya Ufaransa na
hapa tunamnukuu: 'Mimi nataka kufunga saumu nchini Brazil, kwa kuwa ni
Muislamu. Dini tukufu ya Kiislamu inanipa fursa ya kutofunga saumu nikiwa
katika mazingira maalumu kama vile safari na maradhi, lakini pamoja na
kukabiliwa na mashindano ya kombe la dunia nchini Brazil sitaki kufungulia.
Nitaendelea
kufunga saumu ya mwezi mzima wa Ramadhani, Inshaallah', mwisho wa kunukuu.
Licha ya Bacary Sagna wachezaji wengine wengi wanaoozichezea timu za taifa za
Ufaransa, Algeria, Nigeria na Ujerumani wameendelea kusisitiza kwamba watafunga
saumu ya mwezi mtukufu wa Ramadhani licha ya kukabiliwa na mechi ngumu za kombe
la dunia.
Hapo kesho, Nigeria 'Tai wa Kijani' itapimana
misuli na Ufaransa, huku timu ya taifa ya Algeria 'Mbweha wa Jangwani'
itajitupa uwanjani siku ya Jumanne kupambana na Ujerumani katika hatua ya 16
bora.
Inafaa
kuashiria hapa kuwa, hivi karibuni Jiri Dvorak mjumbe mwandamizi wa
Kamati ya Afya ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA alisema kuwa, wachezaji
Waislamu watakaofunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, hawataathirika kiafya wakati
wa kuendelea michuano hiyo nchini Brazil.
No comments:
Post a Comment