![]() |
Wazee wilayani Kilosa |
VIONGOZI wa
vyama vya siasa wilayani Kilosa,mkoani Morogoro wametakiwa kuwashirikisha wazee
kwenye shughuli zao mbalimbali za vyama vyao ili kuwaenzi wakitambua kuwa mzee
ni muhimu wakati wowote si wakati tu wa nyakati za uchaguzi .
Hayo
yamesema hivi karibuni katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilosa kwenye
mkutano wa wadau na wajumbe wa Baraza la wazee wilaya na wazee wa Baraza hilo.
Wazee
hao wameeleza kuwa viongozi wa vyama vya siasa wanapaswa kuwathamini na
kuwatumia wazee wakati wote wa shughuli zao mbalimbali za vyama vyao
wasisubirie mpaka kipindi tu cha uchaguzi wakiwaona kuwa ndio bora zaidi
ili wawapigie kura.
Akizungumzia
hilo katika sera zao vyama vyao katibu wa chama cha CUF wilaya ya Kilosa Sudi
Momborage , Mwenyekiti wa chama UDP Maarufu Salehe Mkambala na
mwenyekiti wa NCCR Magenzi Salumu Mtupe wameeleza kuwa sera za vyama vyao
vinawatahamini wazee na ikiwemo ushirikiano katika haki sawa
kuwaunganisha pamoja ili waweze kutambulika kama makundi mengine .
Naye
katibu wa chama cha mapinduzi CCM wilayani Kilosa Dodo Samba amesema sera ya
Iran ya chama cha mapinduzi.
No comments:
Post a Comment