Monday, June 30, 2014

WAUMINI wa dini wilayani Kilosa watakiwa kuilinda amani ya nchi



 
Viongozi wa dini  wilayani Kilosa
WAUMINI  wa madhehebu mbalimbali ya Dini wilayani Kilosa Mkoani  Morogoro wametakiwa kuitunza na kuilinda  Amani iliyopo hapa Nchini ambaye hiwapa itavunjika itasababisha machafuko katika jamii.


Hayo yamesema hivi karibuni katika tarafa ya kimamba na Selemani  Muhammadi  Madali ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano wa viongozi wa dini mbalimbali wenye lengo la kudumisha amani wilayani Kilosa.

MADALI amesema kuwa amani ni jambo muhimu sana katika jamii hivyo waumini wote wa madhehebu ya dini wahakikishe wanailinda na kuidumisha kwani yapo maeneo mengine Nchi mbalimbali wanaitafuta amani ambayo ikipotea kuirejesha tena ni gharama kubwa.

Naye Mkuu wa baraza la mahusiano ya dini mbalimbali wilayani Kilosa Shekhe Hamza Goma amesema kuwa amani na upendo huja  kwa mshikamano hiwapo waumini wote watailinda na kuishi kwa  kupendana amani iliyopo sasa haitapotea.




No comments:

Post a Comment