Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera |
WASANII mkoani Morogoro wamemuomba Rais Jakaya Kikwete
kumalizia muda wake wa utawala nchini kuikuza tasinia ya sanaa kwa kuwajengea
kituo maalumu cha redio na televisheni itakayokuwa na kazi ya kuibua
vipaji,kutangaza na kuonyesha kazi za wasanii tanzani.
Ombi hilo mbele ya
Mkuu wa mkoa huo Dk.Joel Bendera katika utoaji tuzo ya vipaji ‘Moro town talent
award’ na uzinduzi wa jingo la kuandalia kazi mbalimbali za wasanii ‘Moro Town
Records’ lilikwenda sambamba na ombo la mkoa huo kuwa kitovu cha usanii nchini
kutokana na historia yake katika tasinia hiyo.
Mbele ya mkuu huyo
aliyewakilishwa na Afisa tarafa ya Manispaa Pakala pakala Mulenge,Mkurugenzi
wa kituo hicho na mwenyekiti wa wasanii mkoani humo Mohamed Ngwenje alisema
kilio cha wasanii kupata vituo vya habari ni kuikuza haraka tasinia hiyo na
kuepuka changamoto zilizo kwenye vyombo vya habari.
Akijibu madai hayo
kwa niaba ya Mkuu wa mkoa,Pakalapakala alisema wazo la wasanii hao ni zuri na
linalenga kukabili bomu la ajira kwa vijana na serikali kwa kadri ya uwezo wake
itajitahidi kulitafutia ufumbuzi.
Katika uzinduzi huo
waandishi wa habari,vyombo vya habari,wasanii katika fani mbalimbali,watu
binafsi,taasisi,mashirika na makampuni walitunukiwa tuzo ya umahili katika
sekta yake na Moro Talent award.
WAKULIMA wa zao la mhogo wilayani Kisarawe ,mkoa wa Pwani
washukuru mwezi mtukufu wa ramadhani
kutokana na kuongezeka kwa mauzo ya zao hilo.
Wakiongea na Mbiu ya
Maendeleo wilayani hapo , wakulima hao
wamesema kuwa, kweli mwezi wa ramadahani ni neema kimwili na kiroho kwani
tunashukuru toka jana kumekuwa na
ongezeko kubw ala mazuo ya muhogo kutokana bna wafanyabiashara wengi toka
jijini Dar kuja kwa wingi katika vijiji mbalimbali vinavyozalisha muhogo
wilayani Kisarawe.
Hata hivyo wamesema , ni vyema serikali ikawasaidia
namna bora ya usindikaji wa zao hilo ili kuoingeza thamani kutakoendana na
ukuzaji wa uchumi wa mkulima mdogo.
No comments:
Post a Comment