Mto Ruaha eneo la Ipogolo, Iringa mjini. |
WANANCHI 6,000 katika kata ya
Msangaji,Mawindi,Utengule na Madibira wilayani Mbarali mkoani Mbeya
walioondolewa katika maeneo yao kupisha hifadhi ya taifa ya Ruaha wameazimia
kurudi katika maeneo yao ya awali kama serikali haitakuwa imewapa maeneo
mbadala.
Wanachi hao waliokuwa wakiishi katika vijiji saba vya kata hizo walifikia uamuzi huo juzi kwenye mkutano wao na mkuu wa wilaya hiyo baada ya kuona hakuana juhudi zozote za kuwaokoa kukabiliana na adha ya kuishi katika mazingiara magumu baada ya kufukuzwa.
Baadhi yao akiwemo Salome
Mwakifwamba na Michael Mwanyagile walisema mbali na kuteswa kwa muda mrefu huo
bila hata huruma serikali imeshindwa hata kuwatafutia maeneo mbadala na
kuwalipa fidia zao mapema.
Walisema walihamishwa kinguvu kupisha hifadhi ya Ruaha mwaka
2008 na kumuomba Mkuu wa wilaya kuwasaidia katika suala la fidia
kwani hivi wanamaisha duni kutokana na kulipwa fidia kidogo pamoja na
kutokuwa na mashamba ya kilimo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali
,Gulamhussein Kiffu mbali na kupokea kwa madai hayo aliahidi kuyatafutia
ufumbuzi ndani ya wiki tatu baada ya kuyafikisha kwenye malaka husika na
kurejesha mrejesho.
No comments:
Post a Comment