Waziri wa viwanda,biashara na masoko Dk Abdallah Kigoda |
SERIKALI
imeanza kulia na menejimenti za
viwanda binafsi nchini zinazowatenga watalaamu wanaozalishwa na vyuo vya ngazi
mbalimbali nchini na kuthamini wanaotoka
nje ya nchi kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kuendelea kulitia umasikini Taifa.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa
Viwanda na Biashara Dk.Abdallah Kigoda wakati akifungua kongamano la wanafunzi
wa Vyuo vya elimu ya Juu Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya kwa lengo la
kumwandaa mwanafunzi kutotegemea ajira.
Akizungumzia ongezeko la wataalamu
kutoka vyuo hivyo Dk.Kigoda alisema katika kipindi cha 2010/11 zaidi ya
wanafunzi 130,000 walidahiliwa elimu ya juu na kuwa mwaka 2011/12 kunaongezeko
la wanafunzi zaidi ya 160,000.
Aliwahakikishia
wawekezaji na wamiliki wa viwanda hapa nchini wanauwezo mkubwa wa kuendesha na
kukuza ufanisi kwenye viwanda hivyo nahivyo kuwa na tija kwao na serikali yao
kwa jumla.
Kuhusu kufufua viwanda vilivyokufa
hapa nchini vikiwemo vya nguo,sabuni na vile viwanda vya zana za kilimo
Dk.Kigoda alisema lengo la serikali ni kuhakikisha inavilinda na kuvikuza
kupitia fulsa zilizopo ili kutatua tatizo la ajira kwa vijana.
Kongamano la wanafunzi wa vyuo vya
elimu ya juu Mkoani Mbeya limeandaliwa na chuo kikuu mzumbe kwa udhamini wa
kampuni ya usafirishaji wa ndege ya Fast jet,kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel,mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF na COCACOLA KWANZA.
No comments:
Post a Comment