Soko la Mchikichini,Ilala jijini Dar likiungua |
WANANCHI wa jiji la Dar es
salaam wameiomba serikali kuweka sheria itakayowawezesha wafanyabiashara kupata
bima pindipo watakapo pata majanga ya aina mbalimbali ili kufudia hasara
itayotokana na majnga hayo.
Wakiongea na Mbiu ya Maendeleo
jijini Dar es salaam leo ,wananchi hao wamesema kutokana na ajali ya moto
iliyotokea mwishoni mwa wiki kwenye soko la Mchikichini,Ilala jijini Dar es
salaam ni lazima kuna wafanyabiashara wataoingia katika dimbwi la umaskini
kwani wengi waowanafanya biashara kwa kupata kmikopo toka Taasisi za fedha.
Wamesema ,majibu ya serikali ya mkoa
kupitia mkuu wa wilaya ya Ilala Bwana Raymond Mushi kuwa serikali haina fedha
za kuwawezesha wafanyabiashara waliopoteza mali na mitaji ya biashara zao
kupitia ajali ya moto inaonesha ni kwa namana gani hakuna mikakati madhubuti
toka serikalini na kwa wadau mbalimbali wa maendeleo katika masuala ya bima ili
kumsaidia mwananchi kupata kinga ya kile alichokipoteza.
Mwishoni mwa wiki soko la
Mchikichini ,Ilala,jijini Dar es salaam liliungua kutokana na hitilafu za
umemem na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kwa wafanyabiashara wa soko
hilo.
No comments:
Post a Comment