Ukame ulivyoathiri mazao nchini Kenya |
IMEELEZWA kuwa, huenda Kenya ikakumbwa na uhaba
wa chakula hasa katika maeneo ya vijijini na kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa unaonyesha kuwa, kiwango cha
mvua kati ya Machi na Mei mwaka huu katika maeneo mengi ya Rift Valley kilikuwa
cha chini ikilinganishwa na kiwango chake cha kawaida.
Watabiri wa hali ya hewa wanasema kuwa, kiwango cha mvua
kinatarajiwa kupungua pia katika miezi ya Julai mpaka Septemba hali ambayo
huenda ikapelekea kupungua mno mavuno kati ya Oktoba hadi Februari mwakani.
Wizara ya Kilimo ya Kenya imetangaza kuwa, kiwango cha mazao
kwa mwaka huu bila ya shaka kitakuwa kidogo ikilinganishwa na mwaka jana.
"Kupungua mavuno kunatokana na kupungua uzalishaji katika maeneo
mbalimbali ya Rift Valley hali ambayo imetokana na ukame mtawalia katika miezi
ya Aprili na Mei," imebainisha taarifa ya Wizara ya Kiliomo ya Kenya.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, idadi ya watu wasio na usalama wa kutosha wa
chakula nchini Kenya ilifikia milioni moja
No comments:
Post a Comment