Jeshi la polisi nchini Tanzania |
VIONGOZI wa Vijiji na Kata katika Tarafa
ya Gairo Wilayani humo Mkoani
Morogoro wametakiwa kuunda haraka mabaraza ya kusuruhisha migogoro ya ardhi katika maeneo yao ili kupunguza kesi hizo kwenye mahaka ya ardhi.
Morogoro wametakiwa kuunda haraka mabaraza ya kusuruhisha migogoro ya ardhi katika maeneo yao ili kupunguza kesi hizo kwenye mahaka ya ardhi.
Wito huo umetolewa na Afisa Tarafa wa Gairo Winfred Kipako kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo Viongozi wa vijiji na Kata iliyoandaliwa na Jeshi la Polisi
Wilayani humo.
Kwa mujibu wa Kipako maeneo mengi katika Wilaya hiyo yana migogoro ya ardhi hasa mipaka na mashamba hivyo kusababisha watu kuendelea kuwa masikini kwa kukalia kutatua migogoro hiyo badala ya kufanya shughuli za maendeleo.
Afsa tarafa huyo aliwataka Viongozi hao kuunda mabaraza hayo kwakua ni msingi mkubwa wa haki kwa mwenye eneo badala ya Mahakamani ambako inaweza kusababisha sheria kupindishwa kwa mwenye haki kwa kushindwa kujieleza.
Kwa upande mwingine Jeshi la Polisi Wilayani humo limewataka watendaji
wa Kata kuwapatia ofisi za kudumu askari kata kata maeneo hayo kwani
jeshi hilo limejipanga kuwasambaza askari katika kata.
No comments:
Post a Comment