Mbunge wa Morogoro mjini Abdulaziz Mohamed Abood |
HALMASHAURI
ya Manispaa ya Morogoro imetenga shilingi mil.168 kwa ajili ya ujenzi wa kituo
cha afya cha kata ya Mafisa ikiwa ni kuunga mkono juhudi nguvu kazi za wananchi
waliojitolea kufanikisha hatua za awali za ujenzi huo.
Diwani wa kata ya Mafisa,Francis
Kayenzi alibainisha hayo mwishoni mwa wiki kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika katika mtaa wa Mafisa.
Katika mkutano huo diwani Kayenzi alisema katika bajeti ya
halmashauri hiyo ya miaka miwili shilingi Mi.168 zimeelekezwa kituoni hapo kukamilisha
ujenzi huo na kuwaondolea adha wanachi ya kutembea umbali mrefu kusafa huduma
hiyo.
Hata hivyo akihamasisha michango
zaidi,alisema baada ya kukamilika kwa jengo hilo upo mpango wa kujenga nyumba
za wahudumu wakiwemo madakitari na wauguzi kama kivutio kwa wataalamu hao
kwenye kata hiyo.
Katika mkutano huo Diwani huyo alianisha jinsi fedha hizo zilivyopatikana akimtaja mbunge wa jimbo Abdulaziz Abood aliyetoa shilingi Mil.3.6 na yeye kujitoa shilingi Mil.1.200,000.
No comments:
Post a Comment