Mkuu wa wilaya ya Kilosa |
VIONGOZI wa
vijiji vyote vilivyopo katika Tarafa ya Magole wilayani Kilosa mkoani Morogoro
wametakiwa kuhakikisha wanatumia wadhifa wao kwa kutafuta ufumbuzi wa migogoro
ya wakulima na wafugaji ili kupunguza kasi ya migogoro hiyo hasa katika wilaya
hiyo.
Afisa Tarafa ya Magole Mosos
Nchimbi alisema hayo jana wakati wa akizungumza na gazeti hili na kudai
kuwa endapo viongozi wa vijiji watashiriki kikamilifu katika
kutatua migogoro hiyo bila kupendelea upande wowote wananchi watarudisha
imani kwa viongozi wao ambayo imetoweka kutokana na kukidhiri kwa migogoro
ambayo haitafutiwi ufumbuzi.
Alisema kuwa serikali tarafani humo
imeamua kufanya maamuzi magumu likiwemo kuwatambua wafugaji wakorofi na
kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria,kuweka ulinzi wa doroa hususani kipindi
cha kilimo hadi mavuno na kuviagiza vijiji kuwadhibiti wafugaji kwa kutovuka
maeneo yao hadi mengine.
\
No comments:
Post a Comment