UMOJA wa mataifa umesema kumekuwepo kwa siku mbili za mapigano
katika mji wa Nasir, Sudani ya Kusini.
Msemaji wa Umoja wa matifa amesema
vikosi vya waasi vimeyakalia maeneo ya katikati ya mji huo ambao mapema mwaka
huu ulitumika kama makao makuu ya muda ya kiongozi wa waasi Riek Machar.
Shirika la Habari la Reuters
linaripoti kuwa kambi ya waasi wa Sudani Kusini imesema inatuma ujumbe Ujumbe
wake kuelekea nchini Uganda kufanya mazungumzo na Rais Yoweri Kaguta Museveni
ili kumwomba Museveni kuondoa vikosi vyake vya kijeshi katika Sudani Kusini
ambako vilipelekwa kuisaidia serikali ya Juba.
Mwezi Januari Rais Museveni alisema
vikosi vyake vinamuunga mkono rais wa Sudan Salva Kiir dhidi ya waasi
wanaoongozwa na aliyekuwa makamu wa rais Riek Machar.
No comments:
Post a Comment