Wauguzi wa hospitali Saint Francis Ifakara |
UPANUZI wa kituo cha afya Kibaoni wilayani Kilombero kuwa Hospitali
umeanza kwa kuongeza miundombinu ukitaraji kutumia zaidi ya shilingi
Bil.1.012 kutokana na mapato ya ndani na nje mwaka huu katika
halamashauri hiyo.
Upanuzi huo unaofanyika kwa awamu
mbili unaotaraji kuwanufaisha zaidi ya wanachi 500,000 kwa mwaka wakiwemo
wakazi na wageni wilayani humo ulianza katika mwaka wa fedha 2010/11 ukitaraji
kukamilika 2014/15.
Mganga mkuu wa wilaya Dk Tom Mtoi
alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa kukamilika kwa mradi hua utakao
wanufaisha moja kwa moja zaidi ya wakazi 407,880 unaokwenda sambamba na
ongezeko la watumishi,vifaa tiba,madawa na chumba cha kuhifadhi maiti.
.
Mganga huyo mkuu alisema ujenzi wa
majengo hayo umetekelezwa na mkandarasi na hadi sasa ujenzi wa chumba cha
upasuaji umekamilika na kinatumika na wodi 2,chumba cha kuhifadhia maiti na
jingo la mionzi vimekamilika huku ujenzi wa wodi 3 unaendelea katika hatua ya
awali na linta.
Kuhusu changamoto Dk.Mtoi
alibainisha upungufu wa watumishi wenye sifa kukidhi ikama ya hospitali
akifafanua kuwa kituo kina jumla watumishi 77 kati ya 206 watakaokidhi utoaji
huduma ya afya hospiltalini hapo .
No comments:
Post a Comment