Wednesday, July 2, 2014

OSCAR PISTORIOUS anaugua msongo wa mawazo


Mtuhumiwa wa mauwaji ya mpenzi wake na mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius akiwa mahakamani
RIPOTI  ya daktari wa magonjwa ya akili iliyowasilishwa katika kesi dhidi ya Mwanariadha mashuhuri Afrika kusini, Oscar Pistorius, inaashiria kuwa anaugua msongo wa kimawazo na yumo katika hatari ya kujitoa uhai.

Siku ya Jumatatu, mahakama ilielezwa kwamba Pistorius hana matatizo ya akili wakati alipompiga Bi. Steenkamp risasi .
Anakana kutekeleza mauaji hayo, akieleza kuwa ilikuwa bahati mbaya alipohofia kwamba aliingiliwa nyumbani mwake na mtu asiyemjua.
.
Siku ya Jumanne, Peet van Zyl alisema Pistorius amekuwa mtu anayejulikana kimataifa katika mashindano ya olimpiki kwa walemavu ya mwaka 2012, na alitarajiwa kufanikiwa zaidi.
Mwanariadha huyo aliyekatwa miguu yake miwili, alishindana katika mashindano hayo ya walemavu na ya olimpiki huko London.
Van Zyl amesema huenda Pistorius angejiongezea kipato chake mara tano au sita zaidi.
Aliongeza kwamba ni mfanyabiashara na ana nafasi nyingi kutokana na kusifika kwake. Pistorius akiwa kizimbani Pretoria, ni hakika kwamba aliyatafakari yaliokuwa yakisemwa na Van Zyl kuhusu uwezekano wake kufanikiwa zaidi ambao kwa sasa umebadilika.




No comments:

Post a Comment