Wednesday, July 2, 2014

SARKOZY afikishwa mahakamani kujibu tuhuma za rushwa


ALIYEKUWA Rais wa Ufaransa Nicolaus Sarkozy
RAIS wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, amefikishwa mahakamani mjini Paris, kujibu tuhuma za kutumia nafasi yake vibaya miongoni mwa tuhuma nyenginezo kuhusiana na makosa makubwa ya uchaguzi.

 Sarkozy amepata tena matatani tangu alipopoteza kinga ya kushtakiwa muda mfupi baada ya kushindwa uchaguzi wa urais, uliompelekea rais wa sasa Francois Hollande kushinda mwaka 2012.
Huko nyuma Sarkozy alifikishwa mahakamani kujibu tuhuma  kwamba, ushindi wake wa mwaka 2007 ulitokana na msaada wa dola milioni 70 zilizotolewa na Muammar Gaddafi,  na fedha nyingine kutoka kwa ajuza tajiri wa Kifaransa Liliane Bettencourt mmiliki wa shirika la vipodozi vya I’Oreal. 
Kesi hiyo inaweza kuvunja matumaini ya Sarkozy ya kurejea tena katika ulingo wa kisiasa nchini Ufaransa kwa ajili ya uchaguzi ujao wa rais utakaofanyika mwaka 2017.

No comments:

Post a Comment