IDADI ya watu waliouawa katika maandamano yaliyofanywa
na wananchi wanaopinga mapinduzi ya kijeshi yaliyomuondoa madarakani Muhammad
Mursi huko Misri imefikia 4 baada ya kuuawa msichana mmoja na kujeruhiwa makumi
ya wengine katika mji wa Alexandria.
Waandamanaji wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na askari usalama
katika eneo la Haram huko Giza katika kumbukumbuku ya mwaka wa kwanza wa
mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea mwaka jana nchini Misri.
Raia mwingine aliuawa
katika kitongoji kingine cha eneo la Giza katika mapigano ya askari usalama na
waandamanaji.
Maelfu ya Wamisri jana walifanya maandamano katika miji mbalimbali
ya nchi hiyo kupinga mapinduzi ya kijeshi yaliyoindoa madarakani serikali iliyochaguliwa
na wananchi kwa njia za kidemokrasia ya Muhammad Mursi tarehe 3 Julai mwaka
jana.
Waandamanaji hao walibeba picha za Mursi na kutoa wito wa
kurejeshwa madaraki serikali iliyopinduliwa.
Wakati huo huo Muungano wa Kitaifa wa Kutetea Sheria nchini Misri
umesema una nyaraka zinazothibitisha kesi 54 za kubakwa na kunajisiwa wasichana
ndani ya korokoro za askari usalama wa serikali ya nchi hiyo. Muungano huo
umesema kuwa baadhi ya wasichana hao wamebeba mimba kutokana na kunajisiwa na
askari usalama na kwamba wengine walinajisiwa kwenye magari ya polisi baada tu
ya kukamatwa.
No comments:
Post a Comment