Polisi nchini Uganda wakiwa kwenye doria |
POLISI
nchini Uganda wamedhibiti usalama mjini Kampala kufuatia onyo la
mashambulizi ya kigaidi kupangwa kufanywa katika uwanja wa ndege wa kimataifa
wa Entebe.
Maafisa wa usalama katika uwanja huo,
walisema kuwa onyo la shambulizi hilo lililopangwa kufanyika Alhamisi linapaswa
kuchukuliwa kwa uzito.
Marekani ilitoa tahadhari na kuwashauri
raia wake waliokuwa na nia ya kusafiri kwenda nchini humo Alhamisi kubadili
mipango yao.
Kundi la wanamgambo la Al shabaab
lilishambulia mikahawa miwili mjini Kampala mwaka 2010 wakati wa fainali ya
kombe la dunia nchini Afrika Kusini.
Zaidi ya watu 70 waliuawa katika
mashambulizi hayo, wakati ambapo washambuliaji wa kujitoa manga walipojilipua
wakati mashabiki wa soka walikuwa wakitazama michuano hiyo.
Mikutano kadhaa ya kimataifa inafanyika
nchini humo na lengo la maafisa wa usalama ilikuw akuwahakikishia usalama wao
wajumbe wanaohudhuria mikutano hiyo.
No comments:
Post a Comment